Hi indicator ni rahisi kuitumia na kazi yake ni kuonesha possible reversal na retracement.
TIMEFRAME: M15, M30, H1, H4 ( RECOMMENDED)
Inaweza kutumika kwa scalping na intraday trading.
REVERSAL
– ni kubadilika kwa uelekeo wa price kwa muda mrefu, endapo bullish au
bearish reversal ikitokea trader anaweza akahold position kwa muda mrefu
kulingana na uelekeo wa price, hii itatokea tu kama sellers au buyers
watatoka sokoni baada ya muda mrefu wa ku control market price ( selling
or buying of currency).
RETRACEMENT – hii inatokea endapo price
inabadilisha uelekeo wake kwa muda mfupi tu alafu inaendelea na uelekeo
wa awali. Mfano kama price itakua ipo strong bullish, hii inamaanisha
buyers wananafasi kubwa katika soko kuliko sellers, (buying of
currency). Ila itafika level flani baadhi ya buyers watatoka sokoni, (
some buyers take profit), hapa ndipo inatokea retracement,(bearish
retracement) then other buyers wanaingia sokoni ( other buyers enter to
buy the currency), then price inapanda tena na kua bullish kama awali.
Retracement inaweza kutambulika kwa kutumia FIBONACCI, kwa sababu
FIBONACCI ina calculated mathematical levels ambazo traders wanaamini
kua hizo levels price itaretrace kabla hauijaendelea na uelekeo wa
awali. (nadharia ni kwamba katika market, mambo mengi yanajirudia baada
ya muda flani).
JINSI YA KUTUMIA:
Wakati unatumia hii indicator
kuna vitu lazima uvitambue ili ikupe matokeo mazuri, sababu hii
indicator inafuata sana hivyo vitu, vitu hivyo ni;
• Support na resistance line, ( minor and major support na resistance lines)
• Reversal candlesticks
• Pia ujue trend ya price ipoje kwa wakati huo.
DB
HARMONI SCANNER, ipo kama nyota flani, zenye rangi tofauti, kuna nyota
kubwa yenye rangi kama ya nyano na vinyota flani vidogo vinarangi ya
pink ( sio mzuri kwenye kutambua rangi).
• Ile nyota kubwa mara nyingi kazi yake ni kuonesha reversal, na hizo vinyota vidogo kazi yake ni kuonesha retracement.
•
Naomba nikushauri utrade endapo hizo nyota kubwa zitatokea, coz hizo
zingine zinachanganya sana na zinaweza kutokea bila mpangilio maalumu.
•
Kwa chart yoyete ambayo utatumia hakikisha kama DB HARMINIC SCANNER
itatokea kuonesha reversal basi price iwe imefika katika resistance au
support line,
• Always trade baada ya candle kufunga yaani kama DB
HARMONIC SCANNER imetokea na price imefika katika support au resistance,
basi ni muhimu sana kusubiria candle ifunnge chini ya resistance au juu
ya support line, then ingia candle inayofuata.
• Kama DB HARMONIC
SCANNER imetokea, pirce ipo katika support au resistance na pia kuna
reversal candle, basi hiyo ni best entry point.
• Ni muhimu sana DB
HARMONIC SCANNER ikatokea kwenye TIMEFRAME mbili tofutti, mfano kama
unatrade M30, na imetokea DB basi hakiksha iwe pia imetokea katika H1,
na kama unatrde M15 hakikisha na M30 DB imetokea, pia kama wewe ni H1
trader basi kabla haujafungua trade hakikisha DB HARMONIC SCANNER
imetokea pia katika 1H, na H4. Hiyo ndo njia mzuri zaidi ya kutrade hii
indicator na ikakupa matokeo mazuri.
NOTE: DB HARMONIC SCANNER
inaweza ikatokea mapema sana hata kabla price haijafika katika level
muhimu so kitachotokea itasukumwa mpaka ifike katika level muhimu, ndo
mana nikasema hapo juu lazima uzingatie SUPPORT NA RESISTANCE LINE yaani
zote major na minor S&R. hiyo lazima uwe nayo makini ili kuepuka
kuingia kwenye trade kabla haijafika entry point muhimu.
KAMA
KAWAIDA PRACTICE KWENYE DEMO ILI UIELEWE VIZURI NDO UANZE KUITUMIA LIVE
ACCOUNT, HAKUNA INDICATOR AU SYSTEM YOYOTE INAYOFANYA KAZI ASILIMIA
100%, SO TUMIA RISK MANAGEMENT, NA TRADE WITH TARGET.
Kwa mfano hii USDJPY ilikua inatrend down kuanzai tarehe 8 ikakaa hiyo DB HARMONIC SCANNER, HIYO STAR KUBWA ilitokea H1, na H4 kuonesha reversal na ikaendelea down mpaka soko limefungwa, rejea principle kule know trend. Ila ukiangalia hapo utaona imetokea hapo chini kuonesha kua kutakua na bullish imetokea katika M30. H1, na H4.
Ukiangalia hii EURJPY DB HARMONIC SCANNER imetokea katika M30, H1, na ktika H4 kuna star ile ndogo, na price pia ipo katika resistance line ila bado hakuna confirmation. Rejea principle kule candle should close below resistance or above support line, pia anagalia confirmation candle. (reversal candle).