HOLLY CHANNEL AND HOLLY SIGNAL:

HOLLY CHANNEL AND HOLLY SIGNAL:
Hizi ni inidicator mbili ambazo kwa pamoja ndio zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi, inatumika kwa scalping na day trading.
TIMEFRAME: - M30, H1, H4 (RECOMMENDED)
THE HOLLY CHANNEL- hi ina band juu na chini, ( lower band and upper band) ambazo kazi yake ni kuonesha levels ambazo kama price itafika katika levels hizo basi possibly price itareverse.
Band zote yaani band ya juu na ya chini zina rangi ya bluu na nyekundu, band ya rangi nyekundu ikiwa pana zaidi ya band yenye rangi ya bluu, hii inamaanisha band yenye rangi nyekunda ni muhimu zaidi ,kama price ikifika katika band hiyo basi utegemee kuona reversal. Hii haimanishi band yenye rangi ya bluu sio muhimu hapana, ila inaweza tokea price ikavuka band ya bluu then reversal ikatokea katika band nyekundu. Hili lazima uwe nalo makini wakati unatumia hii indicator.
THE HOLLY SIGNAL- hii ni indicator ambaypo mara nyingi hua inatumika pamoja na holly channel ili ufanisi na signal zenye uhakika. Ipo katika mfumo wa dot, na hua inatoa alert wakati ikiwa inatoa signal, ila usifuat e hiyo alert fuata kitu nitachokuambia hapa.
JINSI YA KUZITUMIA NA KUPATA SIGNAL ZENYE UHAKIKA:
• Ukiweka kwenye chart yako hakikisha umeweka indicator zote kwa pamoja yaani THE HOLLY CHANNEL AND HOLLY SIGNAL.
• Subiri price ifika katika lower band ya rangi ya bluu au rangi nyekundu kama price ipo bearish, au subiri price ifike katika upper band yenye rangi ya bluu au nyekundu kama price ipo bullish.
• Hakikisha wakati price imefika katika lower au upper band basi na HOLLY SIGNAL iwe tayari imekaa wenyewe, ( usifuate alert ya kusell au kubuy inayotolewa na holly signal, alert iwe kama kukupa attention tu)
• Hakikisha baada ya price kufika katika upper au lower band na holly signal ( yaani ile DOT ) imekaa, baada ya candle kufunga basi candle inayofuata iwe ni ya bearish kama price ipo katika upper band au ni bullish candle kama price ipo katika lower band.
• Hakikisha HOLLY CHANNEL iwe imekunja kuelekea juu kama price ipo katika lower band (BULLISH REVERSAL) au imekunja kuelekea chini kama price ipo katika upper band (BEARISH REVERSAL) hii ni muhimu sanaa kutambua muda wote wakati unatumia hii indicator. Sababu kama price itakua ipo katika lower band na THE HOLLY CHANNEL imekunja kuelekea chini hakuna trade hapo, sababu inaonesha strong BEARISH. Pia kama price itakua ipo katika upper band na THE HOLLY CHANNEL ikakunja kuelekea juu hiyo inaonesha strong bullish, hivyo subiri ikupe signal sahihi.
• Kama price itakua imefika katika lower au upper band ya THE HOLLY CHANNEL, hakikisha pia na THE HOLLY SIGNAL ( ile DOT yake) nayo pia iwe imekaa katika band ambayo price imefika. ( Yaani kama price ipo katika bluu band basi na DOT ya HOLLY SIGNAL iwe imekaa katika bluu hivyo hivyo price ikiwa katika band nyekundu basi pia na THE HOLLY SIGNAL iwe imekaa katika band nyekundu.
• Kama ikitokea price imevuka band zote yaani imepita band ya blluu na pia ikaipita band nyekundu, subiri mpaka price irudi katika mfumo wa HOLLY CHANNEL ndio utatrade,kwa kufuata hii indicator. (USITRADE KWA KUTUMIA HIZI INDICATORS PRICE IKUVUKA BAND ZOTE MBILI)
UKIWA UMEHAKIKISHA HAYA YOTE YAMETIMIA BASI INGIA KATIKA TRADE BILA WASI WASI KWA KUFUATA RISK MANAGEMENT NA TARGETED PROFIT, NINA KUHAKIKISHIA UKIFUATA HAYA UTAKUJA KUNISHURU BAADAE.
NOTE: HII NI TECHINICAL INDICATOR USIITUMIA KUTRADE WAKATI WA NEWS.
FANYA MAZOEZI YA JINSI YA KUITUMIA KWENYE DEMO ILI UWE NA UZOEFU NAYO NA KUFUATA SHERIA ZAKE.
HII imetoa signal ya ku buy, waiting for confirmation, then entry
Hapa price ipo katika lower band ila, HOLLY CHANNEL imekunja chini so no signal, coz HOLLY CHANNEL inaonesha strong BEARISH